Thursday, 18 October 2018

 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza  la  Taifa  la  Usalama  Barabarani, Mhandisi  Hamad Masauni, akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jang’ombe, Tiffy Mustafa (kushoto), moja ya kikoti maalumu watakachokua wanavaa wanafunzi watakaoteuliwa  kuwasaidia  wenzao kuvuka barabara  baada ya kuzindua Kampeni  Maalumu  ya  Usalama  Barabarani  na  Udhibiti  wa  Ajali katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo Oktoba 18, 2018 Visiwani Zanzibar.
 Mkurugenzi  wa Taasisi  inayojishughulisha  na  masuala  ya  usalama  barabarani ,Pily  Hamisi  Layda (kushoto)  akimkabidhi  Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi  Hamad  Masauni, mpango kazi wa  Kampeni  Maalumu  ya Usalama  Barabarani  na  Udhibiti wa Ajali iliyozinduliwa  katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo  Visiwani Zanzibar.
 Mwanafunzi  wa  Shule  ya  Msingi  Jang’ombe, Aisha Abdallah Haji, akiuliza swali  linalohusiana  na  uvukaji  wa  barabara kwa watu wenye ulemavu wakati wa  Uzinduzi  wa  Kampeni  Maalumu  ya Usalama Barabarani na Udhibiti wa Ajali katika  Uwanja  wa  Skuli  ya  Jang’ombe, iliyozinduliwa  leo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae  pia  ni  Mwenyekiti  wa  Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), Visiwani Zanzibar
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama  Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati  ya  Uzinduzi  wa  Kampeni  Maalumu  ya  Usalama  Barabarani na Udhibiti  wa  Ajali  katika  Uwanja  wa Skuli ya Jang’ombe, leo Visiwani Zanzibar.

Wanafunzi  wakifurahia  jambo wakati  Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), akizungumza  baada  ya  kuzindua Kampeni  Maalumu  ya  Usalama  Barabarani  na  Udhibiti wa Ajali  katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo  Visiwani Zanzibar. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)


Reactions:

0 comments:

Post a Comment