Thursday, 18 October 2018


MTANGAZAJI wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani DW, Bw. Isaack Muyenjwa Gamba, amefariki dunia mjini Bonn, nchini Ujerumani.

Kwa mujibu wa Mtangazaji mwenzake, Bw. Mohamed Abdulrahman, Gamba alikutwa amekufa akiwa amekaa kwenye kochi nyumbani kwake.

Taarifa zaidi zinasema, Gamba alipaswa awepo kazini Jumanne Oktoba 16, lakini hakutokea, na ndipo wafanyakazi wenzake walipoingiwa hofu na hivyo kuanza kumtafuta kwenye simu zake ambazo nazo zilikuwa hazipokelewi.

“Tulikwenda hadi nyum,bani kwake, na kukuta pazia zikiwa zimefungwa kitu ambacho si kawaida na hata tulipojaribu kupiga simu haikupokewa na ndipo tuliamua kutoa taarifa polisi.” Bw. Abdulrahman alisema.

Taarifa  nyingine zinasema, Polisi walipofika walifuata taratibu za kisheria za ukaguzi, na kuvunja mlango na hapo ndipo walipokuta mtangazaji huyo akiwa amefariki akiwa kwenye kochi.

Issack Gamba kabla ya kujiunga na DW aliwahi kuzifanyia kazi Radio One Sterio, Radio Free Africa na Radio Uhuru.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment