Friday, 13 November 2015

 
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa mjukuu wake marehemu Maryfaustina Yose Mlyambina, (8) iliyofanyika huko Temboni Kimara jijini Dar es Salaam leo Novemba 13, 2015 na kisha mwili wa marehemu kusafirishwa kwenda Magu mkoani Mwanza kwa mazishi. Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, na waombolezaji wengine walishiriki katika ibada hiyo

 
Rais Dkt.John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janet Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya jeneza la mjukuu wao marehemu Maryfaustina Yose Mlyambina(8) wakati wa ibada ya msiba iliyofanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu Temboni Kimara jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mjukuu wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Maryfaustna Mlyambina, aliyefariki Nov 11, 2015. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu zilifanyika leo Nov 13, 2015 Kimara jijini Dar es Salaam, na baadaye msiba huo kusafirishwa kuelekea Mkoani Mwanza kwa maziko

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13,
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwafariji wazazi wa Marehemu Jose Mlyambila na Suzan wakati wa ibada ya mazishi ya mjukuu wake marehemu Maryfaustina Yose Mlambila huko Temboni Kimara jijini Dar es Salaam leo


 Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli, akitoa heshima zake mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Maryfaustina Y. Mlyambina
 Baadhi ya waombolezaji walihudhuria ibada ya misa ya kumuombea marehemu na kutoa heshima za mwisho
 
Rais Mstaafu awamu ya Nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la mjukuu wa Rais John Pombe Magufuli marehemu Maryfaustina Yose Mlyambina aliyefariki akiwa na umri wa miaka nane baada ya kuugua.Ibada misa ya kuuombea marehenu na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika nyumbani kwa wazazi wa Marehemu huko Temboni Kimara jijini Dar es Salaam leo.


Rais Dkt.John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janet Magufuli(wapili kulia), Makamu wa Rais Mhe.Samia Hassani Suluhu(wapili kushoto), Rais Mstaafu awamu ya Nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Said Meck Sadik wakiwa katika ibada ya kuuombea marehemu mjukuu wa Rais John Pombe Magufuli marehemu Maryfaustina Yose Mlyambila iliyofanyika nyumbani kwa wazazi ya marehemu Kimara Temboni jijini Dar es Salaam leo
(Picha zote na Freddy Maro na Muhidin Sufiani-Ikulu)
Reactions:

0 comments:

Post a Comment