Friday, 11 January 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria kupokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 iliyowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019
Maafisa waliokwenda Canada kuipokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 wakilakiwa kwa shangwe Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Isaack Kamwelwe wakipewa maelezo na  Rubani Patrick kuhusu ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 walipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019.(PICHA NA IKULU)
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAMPUNI ya Ndege Tanzania ATCL sasa litakuwa na ndege 11 ifikapo mwakani, baada ya Rais John Pombe Magufuli kutangaza ujio wa ndege nyingine mpya mbili, kuhamisha ndege mbili za Rais na kufufua ndege nyingine moja.
Hayo yamesemwa leo Januari 11, 2019 wakati wa mapokezi ya ndege nyingine mpya aina ya Airbus

Airbus A220-300 kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Ndge hii ya sita sio kwamba ni ya mwisho, Dream liner nyingine yenye uwezo wa kubeba abiria 262 inakuja mwishoni mwa mwaka huu, kwa hiyo Dream liner zitakuwa mbili na Airbuss zitakuwa mbili na zitakuwa zinapishana angani ndani ya Afrika na nje ya Afrika.” Alisema Rais Magufuli na kuongeza, Pia tumenunua Bombardier nyingine itakayowasili nchini mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka ujao, na pia tutakarabati ndege moja aina ya Bombardier na hivyo tutakuwa na ndege 9. Alisema Dkt. Magufuli.
Lakini pia tuna ndege mbili za Rais, nazo zipakwe rangi ya hizi za ATCL nazo zibebe Watanzania Fokker-28 na Fokker-50 ambazo zinabeba abiria 50 nazo zibebe abiria, alisema Rais Magufuli.
Akizungumza zaidi kwenye hafla hiyo, Rais magufuli alisema mafanikio ya nchi kununua ndege hiyo na hivyo kufanya jumla ya ndege sita, ni hatua ya watanzania kujisifu kwani hakuna mfadhili hata mmoja aliyesaidia bali ni watanzania wenyewe.
“Hii ndiyo faida ya kulipa kodi, jukumu la viongozim ni kuhakikisha kodi inayokusanywa na watanzania inatumika ipasavyo na isipotee hata senti tano.” Alisema.
Alisema ndege hiyo ilichelewa kufika lakini kampuni iliyotengeneza imelazimika kulipa dola milioni 1.3 ambazo zitarudi wizara ya fedha.Serikali imenunua jumla ya ndege sita, tatu aina ya Bombardier Q400,  moja aina ya Boeing Dreamliner na mbili ni aina ya Airbus A220-300. Ndege hizo zimekabidhiwa na Kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ili kusimamia uendeshaji wa ndege hizo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment