Saturday, 12 January 2019

NA K-VIS BLOG, ARUMERU
BWENI la wavulana, shule ya sekondari Mlangarini iliyo katika kata Mlangarini Halmashauri ya Arusha Wilaya ya Arumeru, limewaka moto mapema leo Januari 12, 2019.
Taarifa ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Mhe. Jerry Muro aliyoitoa leo, imesema, bweni la shule hiyo mali ya serikali liliungua majira ya saa 1:02 asubuhi.
“Moto ulianza majira ya alfajiri na kuteketeza chumba kimoja kati ya vyumba kumi na nne vya bweni hilo lililokuwa na wanafunzi 84 Hakuna majeruhi wala vifo,” taarifa ya DC Muro ilisema.
Hata hivyo taarifa hiyo ilisema, kuna uharibifu wa mali ikiwemo kuungua kwa  vitanda (double) vitatu (3),magodoro (6), masanduku ya kuhifadhia nguo na madaftari.
“Kutokana na changamoto hiyo nililazimika kufika kwenye eneo la tukio mapema na kuungana na wanafunzi pamoja na wananchi waliojitokeza katika hatua za awali ambapo pia kikosi cha zimamoto kiliwahi kufika kwenye eneo la tukio na kukuta moto umezimwa kwa ( fire extinguisher 11).” Alisema Mhe. Mkuu wa wilaya Jerry MuroReactions:

0 comments:

Post a Comment