Saturday, 4 August 2018

KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo kulia akizungumza mara baada ya kufanya ziara hiyo ya kushtukiza
KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za mamlaka hiyo zilizopo mpakani kwa Tanzania na Kenya eneo la Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga
 KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo kulia akiangalia baadhi ya taarifa kwenye ofisi za mamlaka hiyo zilizopo eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kushoto ni Mkaguzi Mfawidhi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) mpakani mwa Tanzania na Kenya (Horohoro) Thomas Nkondola .
 KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo kulia akionyeshwa  baadhi ya taarifa kwenye ofisi za mamlaka hiyo zilizopo eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya na mkaguzi Mfawidhi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) mpakani mwa Tanzania na Kenya (Horohoro) Thomas Nkondola . mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza
 
  KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo kulia akionyeshwa  baadhi ya taarifa kwenye ofisi za mamlaka hiyo zilizopo eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya na mkaguzi Mfawidhi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) mpakani mwa Tanzania na Kenya (Horohoro) Thomas Nkondola . mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza

  
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA)Agnes Kijo kushoto akimsikiliza kwa umakini Mkaguzi Mfawidhi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) mpakani mwa Tanzania na Kenya (Horohoro) Thomas Nkondola wakati alipofanya ziara ya kushtukiza mpakani hapo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA)Agnes Kijo kushoto akikagua bidhaa mbalimbali zilizokamatwa na mamlaka hiyo eneo la Horohoro wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kulia ni  Mkaguzi Mfawidhi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) mpakani mwa Tanzania na Kenya (Horohoro) Thomas Nkondola
 sehemu ya bidhaa zilizokutwa eneo hilo
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA)Agnes Kijo akisisitiza jambo mara baada ya kumaliza ziara hiyo ya kushtukiza eneo la mpakani mwa Tanzania na Kenya eneo la Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga
   Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa mamlaka hiyo eneo la mpakani mwa Tanzania na Kenya Horohoro na watumisho wengine wanaoshirikiana kufanya ukaguzi  wakati alipofanya ziara ya kushtukiza mpakani hapo.


KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo amefanya ziara ya kushtukiza kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Horohoro wilayani Mkinga na kuridhishwa na utendaji wa watumishi hao huku akiwahaidi kupeleka maabara inayohamishika kwenye kituo hicho ili kuweza kupima dawa za malaria, ukimwi na dawa za kuulia vijidudu.
TFDA na Taasisi za serikali wanatoa huduma ya kufanya ukaguzi wa bidhaa za chakula, dawa,vipodozi, vifaa tiba na vitenganishi kwa ajili ya kuhakikisha vinaingia nchini zikiwa salama na kwamba vimeidhinishwa na mamlaka husika kabla ya kuingia nchini
Agnes aliyasema hayo wakati akiwa eneo hilo mara baada ya kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo wakati wa ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuangalia kama watendaji waliowapa dhamana kwenye vituo vya forodha wanafanya kazi kulingana na sheria, taratibu na miongozi walizowapatia ya kikaguzi kazi kubwa inafanyika kwenye vituo hivyo
Alisema hilo linatokana na eneo hilo kutokuwa na maabara inayohamishika hivyo wataiweka ili waweze kujua dalili na bidhaa kama zinazoingia wakati zinapita mpakani ziruhusiwe au kutokuziruhusu kutokana baada ya kujiridhisha iwapo zinapaswa kufanywa hivyo
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema pia ni kitu kingine ni kuangalia madini joto kutokana na kuwa mpaka huo unaopitisha chumvi kwa wingi sana hapa nchini kwa maana bidhaa uingizwaji wa chumvi wanauzibiti kwa kuangalia ubora na usalama na kujiridhisha kama madini joto yanawekwa kwa hiyo
amelichukua hilo kwa vipimo kwa madini joto vinapatikana vilikuwepo lakini vimekwisha muda wake wa matumizi hivyo ni kuziongeza kwa kuondoa zilizokwisha muda wake wa matumizi.
“Kwa kweli nimeridhishwa na utendaji wa watumishi hapa kwanza kwa sababu ni jumamosi wakaguzi wao wanafanya kazi na taratiibu zinafanyika kama inavyotakiwa huku kila mmoja akiwa kwenye ukaguzi na mmoja ofisini na nyaraka zote zinazopaswa kuwepo za mizigo iliyoingia
zipo na kuwepo kwa ushirikiano na idara nyengine”Alisema
“Nimejiridhisha watumishi wa mamlaka wanafanya kazi kwa waledi mkubwa na vitu nilivyoelezwa vipo kwenye uwezo wetu wa kuvitatua ni wahaidi kuwaletea maabara zinazohamishika kuweza kupima dawa za malaria, dawa za ukimwi na antibayotiki”Alisema
Naye kwa upande wake Mkaguzi Mfawidhi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) mpakani mwa Tanzania na Kenya (Horohoro) Thomas Nkondola alisema bidhaa tofauti tofauti zimekuwa zikikamatwa mpakani hapa ambazo zilikuwa zinapitishwa bila utaratibu kutoka upande wa Mombasa nchini Kenya ambazo zinaingizwa hapa nchini.
Alizitaja bidhaa ambazo wamezikamatwa kuwa ni bidhaa za sukari ambazo zilikuwa zinapitishwa bila utaratibu, mafuta ya nazi ya kupaka, vipondizi vyenye viambato vya sumu ambazo haviruhusiwi kuingizwa nchini ambavyo hivi sasa wapo kwenye utaratibu wa kwenda kuviteketeza.
“Bidhaa zinazopita kwa wingi ni za chakula kwa vipodozi ni mafuta ya nazi ya minara na bidhaa zinazoongozwa ni za chakula na kipindi cha mwezi wa ramadhani tende za debe zisizoruhusiwa zimekuwa zikikamatwa kwa wingi …changamoto nyengine ni wengi wanaoleta bidhaa kutokuwa na
uelewa wa sheria,taratibu za uingizaji wanajaribu kukaa nao kwa lengo la kuwaelimisha wanapaswa kufuata taratibu gani”Alisema.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment