Sunday, 15 July 2018

  Luteni  Khalfan Mturi  kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)akipokea ramani ya Kituo cha umahiri (Centre of Excellence) kwa wachimbaji wadogo wa madini kwa niaba ya meneja wa ujenzi wa SUMA JKT Kanda ya Kaskazini Meja. Daudi Zengo  kutoka kwa Mshauri muelekezi wa mradi huo Bw. Beno Matata kutoka Kampuni ya Inter Consult Ltd, mradi huo unatekelezwa na Wizara ya Madini katika Wilaya ya Handeni, kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini unaotekelezwa na Wizara ya Madini  ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali katika kuwainua wachimbaji wadogo.

 Msanifu majengo wa Kampuni ya Inter Consult Ltd Bw. Beno Matata akieleza mikakati ya kampuni hiyo katika kuhakikisha kuwa inasimamia mradi huo wa ujenzi wa Kituo cha Umahiri kitakachowanufaisha wachimbaji wadogo kinachojengwa Wilayani Handeni ikiwa ni sehemu ya Juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Madini kuinua wachimbajin hao.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bw. Godwin Gondwe akisisitiza umuhimu  wa Kituo cha umahiri  kwa wachimbaji wadogo wa madini Wilayani Handeni kinachojengwa na Wizara ya Madini ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuinua wachimbaji hao katika Wilaya hiyo na maeneo yote ya mikoa ya jirani na Wilaya hiyo.
  Mjiolojia wa Wizara ya Madini Bi. Veronica Nangale akisisisitiza jambo  kwa mkuu wa Wilaya ya Handeni Bw. Godwin Gondwe (hayupo pichani) wakati walipomtembelea Ofisini kwake kabla ya hafla ya kukabidhiwa kwa eneo kitakapojengwa kituo  cha umahiri(Centre of Excellence) kwa wachimbaji wadogo wa madini, hafla hiyo ilifanyika Wilayani Handeni, ujenzi wa kituo hicho unafanyika kupitia  Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini unaotekelezwa na Wizara ya Madini  ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali katika kuwainua wachimbaji wadogo.

  Luteni  Khalfani Mturi  kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akisisitiza jambo mara baada ya kukabidhiwa eneo na ramani ya Kituo cha Umahiri kwa wachimbaji wadogo wa madini kinachojengwa na mkandarasi SUMA JKT, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Wizara ya Madini kuimarisha sekta hiyo na kuwainua wachimbaji wadogo.


Afisa Mipango mji wa Wilaya ya Handeni Bw. Byabato William akisisitiza jambo kwa Luteni  Khalfani Mturi  kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati  wan halfa ya kukagua na kukabidhi eneo litakalotumika kujenga kituo cha Umahiri kinacholenga kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo Wilayani Handeni.(PICHA:FRANK  MVUNGI- MAELEZO).
Reactions:

0 comments:

Post a Comment