Wednesday, 18 July 2018

Msafara wa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ukiwa katika ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano katika kijiji cha Kaole kilichopo wilayani Mvomero mkoaani Morogoro
  Naibu Waziri wa uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe S. Kebwe (wa pili kulia) picha ya maeneo yaliyojengwa minara ya mawasiliano na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete na wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa UCSAF Mhandisi Peter Ulanga
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa ili kushoto) akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu 

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (aliyesimama) Dkt. Kebwe S. Kebwe akiongea na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara yao ya kukagua hali ya mawasiliano mkoani humo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Selemani Kakoso

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (aliyesimama katikati) akiuliza jambo kuhusu hali ya mawasiliano katika kijiji cha Kaole kilichopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro wakiwa kwenye mnara wa Halotel wakati wa ziara yao ya kukagua hali ya mawasiliano mkoani humo. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na wan nne kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Peter Ulanga
  Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Peter Ulanga akitoa taarifa ya upatikanaji wa mawasiliano mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara yao mkoani Morogoro. Waliokaa mbele wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Selemani Kakoso na anayefuata ni Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Kebwe S. Kebwe

 Mwenyekiti wa kitongoji cha Mchanga wa pwani Kaole kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Bwana Henry Daudi akiishukuru Serikali kwa kufikisha mawasiliano kwenye kijiji hicho


Reactions:

0 comments:

Post a Comment