Tuesday, 6 February 2018 Mkurugenzi wa Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Johnson Nyella

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
BENKI Kuu ya Tanzania BoT, inakusudia kufanya mabadiliko ya mfumo wa kuandaa Sera ya Fedha (Monetary policy) ifikapo Machi 2018,  Mkurugenzi wa Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Johnson Nyella, amewaambia waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku tano ya habari za Uchumi, Biashara na Fedha mkoani Mtwara.
Kwa sasa BoT inatekeleza Sera ya Fedha kwa kulenga wingi (quantity) wa shilingi au kwa maneno mengine (ujazi wa fedha) ili ziwe na uwiano muafaka na vitu halisi, alisema mtaalamu huyo nguli wa uchumi wa BoT.
“Mfumo huu tunaotarajia kuuanza utakuwa unaangalia riba kama kiashiria cha mafanikio ya Sera ya Fedha na riba yenyewe itakuwa inaamuliwa na riba ya sera yaani policy rate.” Alibainisha,
Bw. Nyella alisema, riba ya sera itakuwa inaamuliwa na kamati ya Sera ya Fedha au Monetary Policy Committee na ikishaamuliwa BoT itachukua hatua mbalimbali za kisera kuhakikisha kwamba riba iliyoko katika soko la mabenki la kukopeshana inalingana au inakuwa karibu kabisa na ile riba ya sera au policy rate na ndio utaratibu utakaotumika.” Alifafanua.


Mfumo ambao unatumia wingi (quantity) wa fedha, tatizo lake ni kwamba kama kukiwa na mabadiliko ya utashi wa shilingi  katika uchumi, mfumo huo utakuwa unaendelea kuweka ukwasi wa kiwango kile kile cha, malengo ya mwanzo yaliyokuwa yamewekwa, na inaweza kutokea wakati huo shilingi haihitajiki lakini kulikuwa na malengo makubwa ya kuweka shilingi katika uchumi na hivyo kupelekea kuyumba kwa bei katika uchumi, alisema.


“Mnapokuwa mmeweka malengo ya bei au ya riba maana yake  ni kwamba hata kukitokea mabadiliko ya utashi, demand ya shilingi ikipungua mtekeleza sera utaona kwamba riba inaongezeka na hivyo benki itachukua hatua ya kupunguza shilingi kwenye uchumi .” Alisema.


Kinyume chake hitajio (demand) la fedha likiongezeka mtekeleza sera atachukua hatua ya kuongeza shilingi kwenye uchumi ili ziendane na mabadiliko ya utashi (hitajio) la fedha

“Kwa hiyo mfumo unaotumia bei unaubora zaidi kwa vile unauwezo wa kwenda na mabadiliko ya utashi (demand) wa fedha wakati mfumo unaotumia ujazi wa fedha (quantity) unakosoro  na hauwezi kwenda na mabadiliko ya utashi yanayaotokea katika uchumi kwa haraka kiasi cha kutosha.” Alifafanua Bw. Nyella.

Alisema mfumo huo mpya ndio unaotumika kwa sasa na benki nyingi duniani na maamuzi ya kwenda kwenye mfumo huo ni sehemu ya utaratibu ambao BoT umejiwekea wa kuboresha Sera ya Fedha kila wakati lakini pia ni sehemu ya makubaliano na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya kurazinisha  ku harmonize Sera za Fedha katika Jumuiya.

Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusoano wa Umma na Itifaki, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bi. Vicky Msina, (kushoto), akizunhguzma jambo akiwa na Mkurugenzi wa Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Johnson Nyella
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.

Meneja wa BoT, tawi la Mtwara, Bw. Mussa Mziya,(aliyekaa), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa BoT, tawi la Mtwara, Bw.Lucas Mwimo, (wapili kulia) na Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusoano wa Umma na Itifaki, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bi. Vicky Msina
Dkt. Suleiman  Missango, Meneja Msaidizi-Idara ya Utafiti, Kurugenzi ya Sera za Uchumi na Utafiti, BoT, akifafanua baadhi ya masuala ya kiutendaji yaliyokuwa yakitolewa na watoa mada kwenye warsha hiyo.
Mkurugenzi wa BoT tawi la Benki Kuu Mtwara, Bw.Lucas Mwimo akitoammada kuhusu nafasi ya matawi ya BoT, katika utekeelzaji wa majukumu ya benki hiyo.
Meneja wa BoT tawi la Mtwara Bw.Mussa  Mziya akizungumza wakati wa semina ya waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha.
Mtaalamu wa masuala ya mikopo ya nyumba kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Bw.Baraka D. Munisi, akitoa mada kuhusu dhamana ya mikopo ya nyumba (Mortgage Finance)Reactions:

0 comments:

Post a Comment