Tuesday, 16 January 2018

Mweyekiti wa Chama cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO), Bw. Paschal Shelutete, (wapili kushoto), akizunghumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo Januari 16, 2018. Pamoja na mambo mengine, Bw. Shelutete amesema, Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kimeandaa kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Wakala wa Serikali, (MDAs) kitakachofanyika Mkoani Arusha kuanzia tarehe 12-16 Machi 2018. Jumla ya Maofisa 300 wanatarajiwa kushiriki katika kikao hicho. Taarifa kamili ya TAGCO inapatikana hapo chini. Kulia ni Katibu Mkuu wa TAGCO Bw.Abdul Njaidi na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Bw.Rodney Thadeus

Reactions:

0 comments:

Post a Comment