Thursday, 18 January 2018

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), imeokoa karibu nusu ya fedha zilizokuwa zikitumika kuwalipia wagonjwa wa moyo waliokuwa wakisafirishwa kwenda India kwa matibabu ya maradhi ya moyo, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Mohammed Janabi, amesema asubuhi hii Januari 19, 2018 katika mahojiano ya Televisheni.

“Kwa mwaka Serikali ilisafirisha wagonjwa 200 wa matatizo ya moyo kwenda nchini India kwa matibabu, na kila mgonjwa aligharimiwa kwa shilingi milioni 29 ambayo inafanya jumla ya  shilingi bilioni 29.” Alisema

 Akifafanua zaidi Profesa Janabi ambaye ni daktari bingwa mbobezi wa maradhi ya moyo alisema, kwa sasa idadi kama hiyo ya wagonjwa wanatibiwa na Taasisi kwa gharama ya wastani wa shilingi bilioni 17 kwa kila mgonjwa na hivyo kufanya jumla ya shilingi bilioni 17 tu ambazo zinatumika na hivyo kuokoa shilingi bilioni 12 kwa mwaka.” Alisema.

 Profesa Janabi alisema, Taasisi yake imeendelea kupata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka 3 ya uhai wake, ambapo mwaka jana pekee imefanyia upasuaji wa moyo jumla ya wagonjwa 1025 wa ndani na wengine kutoka nje ya nchi.

“Hospitali hii kwa sasa ndio hospitali kubwa kabisa katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki, tunapata wagonjwa kutoka DRC, Malawi, Uganda, na kuna wakati Fulani wa mgomo wa madaktari nchini Kenya, tulipokea wagonjwa kutoka nchi hiyo, kwa hivyo haya ni mafanikio makubwa sana ambayo Serikali inaweza kujivunian kutokana na faida ya uwekezaji kwenye Taasisi hii.” Alibainisha.

 Akizungumzia hali ya afya ya mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti, Profesa Janabi alisema, kwa sasa wamedhibiti tatizo la moyo lililokuwa likiwakabili na wako katika hali nzuri.

 “Tunachoendelea nacho hivi sasa ni kujua ni viungo gani vya mwili mapacha hawa wanashirikiana na viungom gani hawashirikiani ili iwe rahisi kuwatibu katika siku zijazo.” Alisema.

Mapacha hao wenye umri wa miaka 29 wanasomea shahada ya elimu chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU), Mkoani Iringa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment