Thursday, 18 January 2018

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa kutoka Uganda anayekipiga na Wekunu wa Msimbazi Simba, Emmanuel Okwi, amerejea kwenye michuano ya ligi kuu Tanzania Bara almaarufu kama VPL kwa kishindo, baada ya kufunga mabao mawili kati ya manne (4) ambayo Simba imeshinda dhidi ya Sinbgida United, katika pambano lililopigwa uwanja wa Uhusu jijini Dar es Salaam.

Okwi alifunga bao la tatu (3) kufuatia pasi "mchomeko" kutoka kwa Shiza Kichuya, kabla ya kupachika bao la nne kutokana na pasi murua ya Said Ndemla. Kwa matokeo ya leo, Siomba inasalia kileleni mwa msimamo wa VPL, kwa kufikisha jumla ya pointi 29.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment