Monday, 29 January 2018

Mhe. Anthony Mavunde
 
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, (anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Anthony Mavunde, amewataka wamiliki wa pikipiki za abiria Bodaboda, kupitia vikundi kujiunga na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ili kuweza kuhudumiwa endapo waendesha bodaboda watapata madhara ya kuumia au vifo wakati wakifanya kazi zao.
Mhe. Pauline Gekul

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma leo Januari 30, 2018 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa jimbo la Babati Mjini, Mhe.Pauline Gekul katika kipindi cha maswali na majibu ambaye aliyetaka kujua serikali haioni umuhimu wa kuwataka wamiliki wa bodaboda kukata bima kubwa (Comprehensive), ili panapotokea ajali iweze kuwakinga wao na abiria wao.


Akijibu swali hilo Mheshimiwa Mavunde alisema wazo la Mhe. Gekul ni zuri na serikali sio tu ifanye hivyo bali pia inawataka wamiliki na madereva wa bodaboda kupitia vikundi wajiunge na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ili uweze kuwalinda kwa kuwalipa fidia pindi wapatapo madhara wakati wakifanya shughuli zao.

“Najua hiki ni kilio cha wabunge wengi, lakini nitoe rai kwa wamiliki wote wa bodaboda nchini, wakiwemo madereva, wajiunge na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kwa kupitia WCF wanaweza kupata Fidia pindi wapatapo madhara wakati wakitekeleza majukumu yao nah ii itawapunguzia gharama wanazoingia hivi sasa, wapatapo ajali.” Alsiema.

WCF ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ulioanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 5 ya Fidia kwa Wafanyakazi kifungu namba 263 ya mwaka 2015 na moja ya malengo makuu ni kutoa fidia stahiki

kwa Mfanyakazi yeyote kutoka sekta ya Umma na Binafsi Tanzania Bara aliyepatwa na maradhi au majeraha wakati akitekeleza wajibu wake na miongoni mwa Mafao hayo ni pamoja na fao la matibabu, Fidia kwa ulemavu wa muda, (Temporary disability), Msaada wa uangalizi wa kudumu, Msaada wa mazishi kwa mfanyakazi aliyefariki kutokana na kazi aifanyayo, lakini pia Fidia kwa wategemezi wa Mfanyaakzi aliyepatwa na umauti akiwa kazini.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment