Friday, 19 January 2018


ASKARI Polisi wawili wa kikosi cha nkutuliza ghasia, (FFU) mkoani Mbeya, wamefariki katika ajali baada ya gari lao kupinduka, Kamanda wa Poli Mkoani humo, DCP, Mohammed Mpinga amesema leo Januari 19, 2018.

Katika taarifa yake ya kila siku kwa vyombo vya habari, DCP Mpinga amesema, Polisi mkoani Mbeya

imeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu pamoja na ajali za barabarani ili kuhakikisha kuwa wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Hata hivyo Januari 18, 2018 ilitokea ajali hiyo na kupoteza maisha ya askari hao

Alisema ajali hiyo imetokea majira ya saa 10;45 jioni eneo la Iwambi, Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Mkoa humo katika barabara kuu ya Mbeya – Tunduma, ambapo Gari yenye namba za usajili PT 2079 Toyota Land Rover mali ya Jeshi la Polisi Kikosi cha FFU – Mbeya  ikiendeshwa na askari namba G. 3452 PC ADAM (30), Mkazi wa Iganzo ikitokea Mbeya Mjini kuelekea Mbalizi iliacha njia na kupinduka kisha kusababisha vifo kwa askari wawili ambao ni 1. H. 4335 PC MATHEW JAILOS MPOGOLE [26] na 2. H. 1215 PC PROSPER JORDAN CHALAMILA (29).

Aidha katika ajali hiyo, askari 09 walijeruhiwa ambapo kati yao majeruhi wawili wamelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na majeruhi saba wametibiwa na kuruhusiwa. Waliolazwa ni 1. H. 6952 PC KELVIN MARTIN [28] Mkazi wa forest ameumia kichwani na 2. G. 3452 PC ADAM [30] Mkazi wa Iganzo, Dereva.


Aidha majeruhi wengine waliotibiwa na kuruhusiwa ni 1. H. 3929 PC LEONARD MICHAEL [26] ambaye ameumia mkono wa kushoto, 2. H. 469 PC FREDY MBANDE [28] ambaye ameumia mgongoni, 3. H. 948 PC DAVID IBRAHIM [27] ambaye amepata maumivu mwilini, 4. G. 9588 PC MARWA [29] ambaye amepata maumivu mwilini, 5. H. 1325 PC CHRISTOPHER DANIEL MSANGI [26] ambaye ameumia mbavu, 6. H. 6789 PC LUCAS ANDREA MASHALA, [24] ambaye ameumia kichwani na mbavu upande wa kulia na 7. G. 6849 PC HAMIS ALLY [32] ambaye amevunjika mkono wa kulia.


Chanzo cha ajali ni mwendokasi akijaribu kuyapita magari mengine pamoja na utelezi katika barabara. Upelelezi unaendelea. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na majeruhi wamelazwa Hospitalini hapo. Taratibu za kusafirisha miili ya marehemu kwenda nyumbani kwao Iringa zinafanyika.


WITO:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kuwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha madereva kuzingatia udereva wa kujihami hasa kutokana na utelezi na kujiepusha na uendeshaji wa mwendo kasi. Aidha Kamanda MPINGA anatoa rai kwa madereva  kuzingatia sheria na kanuni zote za usalama barabarani.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment