Tuesday, 8 August 2017


Afisa Mwandamizi wa Uhamiaji, SACI Fulgence Mutarasha (wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi juu ya ulipaji wa visa kwa wasafiri wanaotoka nje ya nchi kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), baada ya eneo hilo kutembelewa na Manaibu wa Wizara za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Mhandisi Edwin Ngonyani (wa pili kulia), Wizara ya Maliasili na Utalii – Mhandisi Ramo Makani (mwenye miwani) na Wizara ya Mambo ya Ndani – Mhe. Yussuf Masauni (wa tatu kulia).


Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uzingatiaji Viwango cha Mamlaka ya Viwanja vha Ndege Tanzania (TAA), Bw Paul Rwegasha (watatu kutoka kulia) akitoa maelezo mbalimbali kwa Manaibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mhe Yussufu Masauni (wa pili kulia); Wizara ya Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani (mwenye suti nyeusi) na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (wa tatu kutoka kushoto), walipotembelea jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).


Meneja Msaidizi wa Huduma kwa Abiria wa Forodha kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Damas Temba (wa kwanza kulia), akitoa maelezo kwa Manaibu wa Wizara za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Mhandisi Edwin Ngonyani (wa kwanza kushoto), Wizara ya Maliasili na Utalii – Mhandisi Ramo Makani (mwenye miwani) na Wizara ya Mambo ya Ndani – Mhe. Yussuf Masauni (wa tatu kulia) walipofanya ziara ya kukagua miundombinu ya JNIA.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment