Tuesday, 1 August 2017

Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya  SUNSHINE GROUP, Betty Mkwasa wakati alipotembelea  mtambo wa kusafisha dhahabu wa Sunshine Mining Limited uliopo Chunya Agosti 1, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka  Dennis Dillip ambaye ni Mjiolojia  kuhusu mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni  ya Sunshine Mining Limited uliopo Chunya wakati alipoutembelea Agosti 1, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakipata Maelezo kutoka kwa  Afisa  Madini wa Mkoa wa Mbeya Mhandisi Said Mkwawa kuhusu taarifa za  Kampuni ya Sunshine Gold Mininga Limited  wakati alipotembelea mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni hiyo wilayani Chunya  Agosti 1, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia wimbo maalum unaozungumzia utendaji wa serikali ya  Awamu ya Tano ulioimbwa  na Kwaya maarufu ya Kiwete  katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri  Mkuu kwenye uwanja wa Sabsaba mjini Chunya Julai 1, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sabasaba  mjiini Chunya Agosti 1, 2017.  Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Kigoda kutoka kwa Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaso ikiwa ni ishala ya kusimikwa kuwa Chifu wa makabila ya  Wasafa na Wakimbu katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Chunya Agosti 1, 2017. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU ATEMBELEA MTAMBO WA KUSAFISHA DHAHABU CHUNYA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea na kujionea mtambo wa kisasa wa kusafisha  dhahabu kwa asilimia  99 unaomilikiwa na kampuni ya Sunshine Group uliopo katika kata ya Matundasi wilayani Chunya mkoani Mbeya.

Ametembelea mtambo huo leo (Jumanne, Agosti 1, 2017) wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya na kusema kuwa mtambo huo ni wa kwanza kuweza kusafisha dhahabu kwa kiwango hicho hapa nchini.

Amesema kwa Tanzania kampuni ya Sunshine Group ndiyo yenye mtambo wa kuweza kusafisha dhahabu na kufikia asilimia 99 ukilinganisha na makampuni mengine yanayomiliki migodi.

Pia Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuwekeza katika mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuchenjulia makinikia ili kuweza kusafirisha dhahabu halisi.

Naye Ofisa Madini Mkoa wa Mbeya, Mhadisi Said Makwama amesema dhahabu inayosafishwa katika mtambo huo ikipelekwa nje ya nchi inaingizwa sokoni moja kwa moja tofauti na migodi mingine.

Mhandisi huyo alisema Sheria mpya ya Madini imesaidia Serikali kupata kodi ya juu itokanayo na Mrabaha wa asilimia 6 na ‘clearance and inspection fee’ ya asilimia moja ya thamani ya madini  yanayosafirishwa ukilinganisha na mrabaha wa awali wa asilimia nne.

Uzalishaji uliofanyika kwa mwezi Julai tu Serikali imepata mrabaha wa sh. milioni 333 ukilinganisha na sheria ya zamani Serikali ingepata shilingi milioni 191. Sheria mpya imewezesha Serikali kupata mapato zaidi ya sh. milioni 142. Awali ilikuwa inapata  sh. milioni 191 kwa gramu 52. 518 kwa mgodi mmoja wa Sunshine.”

Kwa upande wake mbunge wa Chunya, Mheshimiwa Victor Mwambalaswa ameiomba Serikali kukubali maombi ya Kampuni ya Sunshine ya kujenga mtambo wa kuchenjulia mabaki ya mchanga wa dhahabu wilayani Chunya ili kuweza kuongeza fursa za ajira, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linashughulikiwa.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sunshine Group Bw Leo Le alisema kampuni ya Sunshine Group ni ni miongoni mwa makampuni makubwa kutoka nchini China yaliyowekeza Tanzania, ambapo thamani ya uwekezaji wao ni zaidi ya Dola za Marekani milioni 100.


(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 1, 2017
Reactions:

0 comments:

Post a Comment