Monday, 7 August 2017

NA K-VIS BLOG/MASHIRIKA YA HABARI
 WAKENYA Milioni 19.6 ambao wamejiandikisha kupiga kura leo Agosti 8, 2017 wataamua nani awe rais wao wa tano kati ya Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, anayepeperusha bendera ya Jubilee na Raila Odinga ambaye anapeperusha bendera ya muungano wa NASA, ambapo maeeno mengi ya Kenya wapiga kura wameanza kupiga kura ambapo vituo vilifunguliwa mapema saa 12 asubuhi.
na upigaji kura utaendelea hadi saa 11 jioni, na matokeo ya kura yatatangazwa baada ya siku saba.
Jumla ya vituo  40,883 vimetengwa nchi nzima na kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya kimataifa, wapiga kura wameanza kufika vituoni tangu saa 7 usiku licha ya baridi kali ambayo imefika nyuzi joto 15c.
Rais Uhuru Kenyatta, (55), anagombea muhula wake wa pili na wa mwisho na anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mwanasiasa mkongwe Raila Odinga (72) anaeongoza muungano wa upinzani NASA na kwa sasa anawania nafasi hiyo ya Rais kwa mara ya nne.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment