Thursday, 3 August 2017Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewasili mjin I Tanga leo Agosti 3, 2017 tayari kuungana na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwenye uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa bomba la mafuta litakalotoka Hoima nchini Uganda kuja Tanga nchini Tanzania Jumamosi Agosti 4, 2017. Pichani Rais Magufuli aambaye kama kawaida yake alisafiri kwa njia ya barabara kutoka jijini Dar es Salaam, alipata wasaa wa kusalimiana na wananchi huko Msata, Kabuku, Hale na Muheza. Pichani Rais akiwapungia wananchi wa Mkata waliosimama pembeni ya  barabara kuu ya Chalinze-Segera  mara baada ya kumaliza kuhutubia katika kijiji cha Mkata mkoani Tanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja ya wakazi wa Hale mkoani Tanga mara baada ya kuhutubia katika eneo hilo.


Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tanga akiwemo Wabunge na wakuu wa Wilaya wakipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia Mkata mkoani Tanga.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza   Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Bi.Khadija Juma mara baada ya kusoma ujumbe ulioandikwa kwenye sare aliyovaa mama huyo.Wananchi wa Muheza wakimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kufika katika eneo hilo la mjini akiwa njiani kuelekea Tanga. (PICHA NA IKULU)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela kabla ya kuwahutubia wananchi wa Hale mkoani Tanga.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment