Tuesday, 8 August 2017

IKITAMBULISHA kikosi chake kipya ilkichosajili kwa ajili ya msimu huu wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/2018 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ya Dar es Salaam ikionyesha kandanda safi na lenye mpangilio, imewafunga mabingwa wa ligi kuu ya Rwanda, Rayon Sport bao 1-0. Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na timu hiyo na kuonyesha kandanda safi na ya kiuvutia ni pamoja na kiungo wa zamani wa Yanga, raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima na mshambuliaji wa xzamaniwa Simba, Mganda Emmanuel Okwi.
 Gyan
 Okwi
 Kocha Mkuu Omong
 Jackson Mayanja
 Manara
 Msemaji wa Simba Haji manara Akiwatambulisha Nahodha Msaidizi Mohamed Husein kwa Mashabiki wa Simba Akiwa Sambamba na Nahodha wa Timu hiyo Mwanjali
niyo
Hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao hilo moja na kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko Simba ikimuingiza kiungo wao hatari Haruna Niyonzima kipenzi cha wana Yanga aliyehamia Msimbazi na alionesha uhodari mwingi kwa kuuchezea Mpira kwa madaha.
IMG_5204
Kama Simbaa wangekuwa makini wangeweza kutoka na ushindi mnono kwani mshambuliaji wao hatari John Bocco aliweza kukosa nafasi mbili za wazi akiwa yeye na golikipa hadi mpira uanaisha Simba wameibuka na ushindi wa bao 1-0 na kusherekea vizuri siku yao ya Simba Day ambayo imetimiza miaka tisa tangu kuanzzishwa.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment