Monday, 7 August 2017


Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu ya Simba na mtoto  Mwamvita Hassan ambaye timu hiyo imemlipia shilingi milioni mbili kwa ajili ya gharama za upasuaji wa Moyo. Msaada huo ni sehemu ya sherehe za Simba Day, zinazofikia kilele Agosti 8, 2017 kwa timu hiyo kutambulisha kikosi chake kipya kwa msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi pamoja na wachezaji wa timu ya Simba mara baada ya kumaliza ziara yao ya kuitembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akieleza umuhimu  wa mchezaji kupima magonjwa ya moyo ili kuepuka  kupata madhara ya ugonjwa huo wawapo uwanjani kwa baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu ya Simba waliotembelea Taasisi hiyo leo Agosti 7, 2017.


Nahodha wa timu ya Simba Method Mwanjali akimkabidhi hundi ya shilingi milioni mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo za mtoto Mwamvita Hassan (wa pili kulia) ambaye anatibiwa katika Taasisi hiyo. Kulia ni Msemaji wa timu ya Simba Haji Manara.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiagana na mchezaji mpya wa Simba, Haruna Niyonzima mara baada ya ziara ya timu ya Simba kwenye taasisi hiyo kukamilika. Kulia ni Katibu Mkuu wa Simba Dkt. Anord Kashembe.


Wachezaji wa timu ya Simba Haruna Niyonzima na Nicholaus Gyan wakimsikiliza  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alipokuwa aliwaeleza madhara yatokanayo na magonjwa ya Moyo anayoweza kuyapata mchezaji awapo uwanjani. Baadhi ya viongozi wa timu hiyo pamoja na wachezaji walitembelea JKCI leo kwa ajili ya kuona huduma wanazozitoa pamoja na kukabidhi hundi ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa mtoto Mwamvita Hassan.


Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Godwin Sharau akiwaeleza wachezaji wa timu ya Simba aina mbalimbali za upasuaji wa moyo kwa watoto wanazozifanya wakati baadhi ya wachezaji wa timu hiyo pamoja na viongozi  walipotembelea Taasisi hiyo leo.Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya Simba waliotembelea Taasisi hiyo leo.(PICHA NA JKCI)
Reactions:

0 comments:

Post a Comment