Saturday, 5 August 2017


 Rais John Pombe Magufuli, akipeana mikono na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda kuja Chongoleani mkoani Tanga leo Agosti 5, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa mkono Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza kuhutubia katika  sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania ambapo aliwataka wananchi wa nchi za Uganda na Tanzania kuutumia mradi huu kwa manufaa ya nchi hizi mbili.Rais wa Uganda  Yoweri Kaguta Museveni akiongea wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania ambapo alisema mradi huu uwe chachu ya kuimarisha uchumi ili kuwa na jumuiya imara ya Afrika Mashariki.


Waziri wa Nishati wa Uganda Irene Muloni akiongea wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania aliwapongeza Rais Magufuli na Rais Yoweri Museveni pamoja na timu ya wataalamu waliofanikisha hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa Mradi wa huu.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na wasanii waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania


Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimpa mkono Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza kuhutubia katika  sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakiwa katika picha za pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.(PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO)

 Rais John Pombe Magufuli, akipeana mikono na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda kuja Chongoleani mkoani Tanga leo Agosti 5, 2017.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment