Saturday, 5 August 2017

KIT1
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amepokea Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye tamani ya zaidi ya shilingi Million 300 kutoka kampuni ya mafuta ya Camel Oil iliyoamua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha sekta ya Afya.
Akizungumza baada ya kupokea Vitanda hivyo, Makonda amesema amedhamiria kuhakikisha changamoto zote zinazoikabili sekta ya Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam zinamalizika lengo likiwa ni kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya.
“Sitaacha kutafuta kwa ajili ya Wananchi wa Dar es salaam, nitabisha hodi kila panapostahili ilimradi Wananchi wangu wawe wanapata huduma za Afya katika mazingira mazuri. Na siku moja waone kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. John Magufuli. Sisi tunataka Maendeleo na maendeleo hayana chama,dini wala kabila. Jukumu la kuuendeleza Mji huu wa Dar es salaam ni jukumu letu sote kama wakazi na wananchi wa mkoa huu” Alisema Makonda.
Makonda amesema anatamani siku moja kila mama anaekwenda kujifungua alale kitanda kimoja mwenywe na sio kama ilivyo sasa ambapo wanatumia kitanda kimoja kina mama watatu hadi wanne
Reactions:

0 comments:

Post a Comment