Friday, 4 August 2017

003
Mgeni rasmi Mkurugenzi  wa Huduma za Uuguzi Taasisi ya MOI, Bi. Flora Kimaro, (katikati), akikakata utepe kuashiria kuanza kwa shughuli za maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani iliyokwenda sambamba na kutoa huduma za kiuchunguzi kwa wagonjwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili leo Agosti 4, 2017.

001
Mgeni rasmi, Flora Kimaro ambaye ni Mkurugenzi  wa Huduma za Uuguzi Taasisi ya MOI akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili leo. Pamoja na maadhimisho hayo Chama cha Wakunga Nchini (TAMA) kimepongezwa kwa kutoa huduma za afya ambapo watu wanapima afya leo katika hospitali hiyo. Siku ya Wakunga Duniani huadhimishwa Mei 5, kila mwaka, lakini TAMA tawi la Muhimbili imeamua kuadhimisha siku hii katika wiki ya unyonyeshaji duniani.
002
Baadhi ya wananchi waliofika katika siku ya maadhimisho hayo wakimsikiliza mgeni rasmi.
005
Mgeni rasmi pamoja na baadhi ya maofisa wa Muhimbili wakiwamo wakunga wakielekea meza kuu leo.
004
Mmoja wa wauguzi, Gladisia Kessy akimpima afya mmoja wa watu waliofika Muhimbili leo kwa ajili ya kushuhudia maadhimisho hayo.
006
Baadhi ya watu wakifuatilia maadhimisho hay oleo.
007
Maofisa wa Muhimbili wakiwamo wakunga wakiwa katika picha pamoja leo.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment