Monday, 7 August 2017

WhatsApp Image 2017-08-04 at 16.52.06
Mahakama Kuu Tanzania, imetupilia mbali ombi la Yusuf Manji kutaka apatiwe dhamana katika kesi yake inayomkabili ya kuhatarisha usalama wa taifa.
Ombi hilo lilifunguliwa na mawakili wa Manji, lakini Mahakama Kuu imepitisha uamuzi wa kulitupitia mbali ombi na kumresha Manji katika korokoroni ya gereza la Keko jijini Dar es Salaam.
Mawakili wanaomtetea, waliamua kufungua ombi hilo baada ya Manji kunyimwa dhamana katika Mahakama ya Kisutu katika kesi inayomkabili wakiiomba mahakama hiyo impatie dhamana mteja wao.
Manji ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya soka ya Yanga, amejikuta matatani hivi karibuni ambapo anadaiwa kutenda maosa mbalimbali ambayo kimsingi hayana dhamana.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment