Wednesday, 9 August 2017

 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Banda la maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Makamu wa Rais alipokelewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Rose J. Msoka(kulia).

NA MWANIDHI WETU, LINDI
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA kwenye maonesho ya NANE NANE yaliyofikia kilele Jumanne Agosti 8, 2017 mjini Lindi na kufurahishwa na ufanisi mkubwa katika kuunganisha mifumo ya Serikali yenye kulenga utoaji huduma bora na kurahisisha shughuli ya Utambuzi kwa wananchi.
Mheshimiwa Makamu wa Rais ametembelea Banda la NIDA akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha maonesho ya sikukuu ya Wakulima Kitaifa maarufu Nanenane yaliyofanyika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. Mhe. Samia aliambatana na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dtk. Charles Tizeba.
Katika maonesho hayo NIDA ni miongoni mwa Taasisi zilizofanya vizuri na kupata ushindi katika makundi 15 yaliyotangazwa washindi.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment