Saturday, 5 August 2017

KATIKA hatua ambayo haikutarajiwa, Rais John Pombe Magufuli, (JPM), leo Agosti 5, 2017 amewapatanisha Mkurugenzxi wa vipindi wa Clouds Media Group, (CMG) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, baada ya kuwaita jukwaani na kuwataka wapeane mikono. Rais alichukua hatua hiyo, wakati akihutubia kwenye hafla yab kihistoria ya uzinduzi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda, kuja kijiji cha Chongoleani kunakopatikana bandari ya Tanga.
Rais Magufuli na Rais Yoweri Kaguta Museveni, ndio walioweka jiwe la msingi kwenye hafla hiyo.
 
Reactions:

0 comments:

Post a Comment