Tuesday, 1 August 2017


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akikabidhiwa kipeperushi na Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na kuzuia uhalifu na ajali, (UAC), Bw. Elliot Andrew wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya namba ya dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa taarifaza majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine.

Anayeshuhudia ni Naibu Kamishna Rasilimali Watu wa Jeshihilo, Billy Mwakatage (kulia). Uzinduzi huo umefanyika leo Agosti 1, 2017 makao makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam. (PICHANAJESHI LA ZIMAMOTONAUOKOAJI).

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizindua namba hiyo.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya namba ya dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa taarifaza majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Wengine ni Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na kuzuia uhalifu na ajali (UAC), Bw. Elliot Andre na Naibu Kamishna Rasilimali Watu wa Jeshihilo, Billy Mwakatage (kulia). Uzinduzi huo umefanyika leo Agosti 1, 2017 makao makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam.

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizindua namba hiyo.
 Baadhi ya maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliohudhuria kwenye hafla hiyo.
Kamishna Jenerali na Mafisa wa jeshio hilo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau hao wa sekta ya uokozi na kuzuia uhalifu.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment