Tuesday, 1 August 2017Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akionyesha Jarida la Mpango Mkakati la Shirikisho la Masumbwi Tanzania (BFT) mara baada ya kufanya nao mazungumzo katika Ofisi za Wizara 01 Agosti, 2017 Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaana Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewaahidi Shirikisho la Masumbwi Tanzania (BFT) kuwatatulia kero ya eneo la kufanyia mafunzo pamoja na ofisi ambalo limekuwa likiwakabili kwa muda mrefu zikiwemo na changamoto nyingine za Shirikisho hilo.
Mhe. Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Viongozi na wajumbe mbalimbali wa shirikisho hilo ikiwa ni sehemu ya kutambua utendaji kazi wao na changamoto zinazowakabili ili ziweze kutatuliwa.
Dkt. Mwakyembe amesema kwamba, kutokana na tatizo la ukosefu wa eneo rasmi la ofisi na sehemu ya kufanyia mafunzo, yeye atawasiliana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ili kuona namna gani wanaweza kupata eneo kwa ajili ya kulisaidia shirikisho hilo kwa ajili ya kujenga ofisi na eneo la kufanyia mazoezi.
Sambamba na hilo, ameupongeza uongozi wa shirikisho hilo kwa kazi wanazozifanya na kuwataka wazidi kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) hususani katika kupeana taarifa zinazohusu maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini.
“BFT jitahidini muwe na ushirikiano wa karibu na Baraza la 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment