Friday, 11 August 2017

Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM,na Diwani wa Kata ya Sambasha  mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya (aliyevaa suti nyeusi)akiwa nje ya mahakama mara baada ya kuachiwa kwa dhamana kutokana na kesi inayomkabili.(Picha na
Vero Ignatus Blog)
.
 NA VERO IGNATUS, ARUSHA
Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha leo Agosti 11, 2017 imemsomea mashtaka mawili aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini .
Miongoni mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo ni pamoja na kosa la tuhumiwa ya kujifanya Afisa Usalama wa Taifa, (TISS), huku kosa lingine ikiwa ni kugushi moja ya
nyaraka za serekali(kitambulisho ).
Akisoma mashtaka hayo mahakamani hapo,wakili wa serekali Penina Joakim  amesema kuwa Mnamo Mei 18 katika hotel ya Skyway iliyopo makao mapya jijini Arusha Mshitakiwa
alijitambulisha kama Afisa utumishi wa idara ya usalama wa taifa na kufanya Utapeli .
Wakili Penina alitaja kosa la pili ambalo
Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya alisomewa kuwa ni kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa Taifa kilichokuwa kikisomeka Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania idara ya usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya kikosi maalumu Agent (undercover), chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa ni kinyume cha kisheria .
Hata hivyo mara baada ya kusomewa
mashtaka hayo mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka na ndipo Hakimu Mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Nestory Barro alisema dhamana ipo wazi iwapo wadhamini watakidhi vigezo vinavyotakiwa na mahakama
hiyo.


Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM,na Diwani wa Kata ya Sambasha  mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya (aliyevaa suti nyeusi)akizungumza na vyombo vya habari
nje ya mahakama.Picha na Vero Ignatus Blog.

 Akizungumza na mwenyekiti wa CCM katika kata ya Sambasha Lesion Letionoki Njoki.Picha na Vero Ignatus
Blog.

 Akisalimiana na wananchi wa kata ya Sambasha mara
baada ya kuachiwa kwa dhamana.Picha na Vero Ignatus Blog.
 
Reactions:

0 comments:

Post a Comment