Thursday, 13 July 2017NA K-VIS BLOG, Lindi
WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea kituo cha kupoza na kusafirisha umeme kilichoko kijiji cha Mahumbika Wilaya ya Lindi na kusema tatizo la kukatika umeme mikoa ya Lindi na Mtwara kumalizika kabisa ujenzi wa kituo hicho utakapokamilika.

Waziri Mkuu ambaye alitembelea mradi huo jioni ya Alhamisi Julai 13, 2017, alisema mradi huo utakapokamilika, uwezo wa kusafirisha umeme utafikia Msongo wa Kilovoti 132, kutoka Msongo wa kilovoti 32 za sasa.

Waziri Mmju alisema azma ya Serikali kupitia Shirika lake la umeme TANESCO ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme kote nchini ili Watanzania wapate umeme mwingi na wa uhakika utakaosambazwa hadi vijijini na kwa gharama nafuu.

“Mikoa wa Lindina Mtwara ilikuwa na shida kubwa ya kukatika kwa umeme mara kwa mara mradi huu ni mkombozi kwa wana Lindi na Mtwara, tunawakaribisha wawekezaji waje kuwekeza kwa sababu sasa nishati ya umeme ni ya uhakika.” Alisema Mhe. Majaliwa.
Alisema mradi huo umegharimu kiasi cha Sh. bilioni 16 fedha za walipa kodi wa Tanzania.

Aidha Waziri Mkuu alisema kwa waannchi wa vijijini ambao hawana umeme umeme  serikali ya awamu ya tano itafanya uzinduzi wa miradi ya umeme vijijini REA mwezi huu Julai    katika  mikoa ya Lindi na Mtwara.
tunataka kila mwananchi awe na umeme, kwa sasa serikali imeshusha gharama za kufungiwa umeme , huduma hii sasa itapatikana kwa Sh. 27,000 tu. Hivyo hakuna mwananchi atakayekosa kuunganishiwa umeme . Naye Mhandisi Kahitwa Bishaija ambaye ni Msimamizi wa Mradi huu wa ujenzi wa njia ya 132kv Mtwara -Lindi pamoja  na kituo cha Kupoza umeme cha Maumbika alisema  mahitaji ya umeme kwa mkoa wa Lindi ni Megawatt 5 lakini kukamilika kwa mradi huo Lindi sasa itapata Megawati 90 za umeme utakaosafirishwa kutoka Mtwara hadi hapa Maumbika kasha kusambaza kwa wateja  katika njia tano tofauti  hivyo kupunguza athari za kukatika katika kwa umeme.
“Hapo awali tulikuwa tunategemea njia moja tu ya kusambaza umeme nai kitokea hitilafu yoyote wateja wetu wote wanaathirika, lakini baada ya mradi huu kukamilika hakutakuwa na tatizo hilo tena.” Alisema Mhandisi Bashaija.
Mhandisi huyo alisema mradi umekamilika kwa asilimia 95 na kwamba kinachofanyika kwa sasa ni kuwasha mitambo kwa majaribio klakini pia kufunga baadhi ya vifaa vya kudhibiti mfumo wa umeme.
Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amesema mradi huu utawezesha kuimarika kwa upatikanaji wa umeme wa uhakika na hivyo kuwahakikishia Watanzania kuwa safari ya kuelekea ujenzi wa uchumi wa viwanda ni ya uhakika.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye. 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Mhe. Waziri Mkuu, akikagua mradi huo wa Mahumbika.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Jafary Msuya, wakati alipotembelea mradi huo unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Ferdinand Mwinje, wakati akikagua mradi huo unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na wananchi, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme wa Mahumbika, unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)​


Reactions:

0 comments:

Post a Comment