Friday, 14 July 2017

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Amina Mohammed akiwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Kenyata kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga. Dkt. Mahiga alipokea ujumbe huo leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

katika mazunguzmo yao, Mawaziri hao wamekubaliana na pendekezo la kuunda Kamati itakayoongozwa na wao wenyewe ambayo itakuwa na jukumu la kutafuta suluhu ya haraka inapotokea migogoro ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment