Sunday, 16 July 2017


index
Na Tiganya Vincent- RS-Tabora
WAKUFUNZI  wametakiwa kutumia lugha zinazosaidia wanachuo kujengeka udilifu  badala ya kuwakatisha tamaa kwa maneno ambayo yanawavunja moyo wa kuendelea kujifunza na kubadili tabia zao endapo zinakuwa hazina tija  katika maendeleo yake ya kitaaluma.
Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbawara wakati wa ziara ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chuo Cha Reli kilichopo Tabora.
Alisema kuwa lazima wakufunzi  watambue wapo pale kwa ajili ya wanachuo  kwani wasingekuwepo nao wasingekuwa na kazi ya kufanya.
Profesa Mbawara aliongeza kuwa Mkufunzi Mzuri ni yule anapoona maendeleo ya mwanachuo wake hayaridhishi ni jukumu lake la kukaa naye na kumsikiliza na kisha kumshauri njia nzuri ya kumuondoa pale alipo na kwenda mbele zaidi.
Aliwataka wanafunzi kuwa waadilifu na kusoma kwa bidii na kuongeza kuwa uadilifu uanzia katika shule na sio kazini.
Kwa upande wa Wanachuo hao waliomba Serikali iwasaidie kupatiwa mikopo na fedha mafunzo kwa vitendo kama vilivyo wengine wa Vyuo vingine hapa nchini.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment