Wednesday, 12 July 2017


 Mwanasoka wa zamani wa timu ya Manchester United ya Uingereza, ambaye sasa amejiunga na timu ya Everton pia ya nchini humo, Wayne Rooney, (wakwanza kushoto), akiongozana na wachezaji wenzake wakati wakiingia uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jioni hii Julai 12, 2017 kwa ajili ya kufanya mazoezi mepesi kabla ya kuwavaa mabingwa wa kombe la SportsPesa 2017, Gormahia ya Kenya hapo Alhamisi Julai 13, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WABONGO watapata fursa ya kumuona "Live" mwanasoka nyota wa Uingereza aliyejiunga na Everton akitokea kwa mashetani wekundu, Manchester United, Wayne Rooney katika mchezo maalum dhidi ya mabingwa wa SportsPesa Super Cup 2017, timu ya soka ya Gormahia ya Kenya.
Rooney ndiye alikuwa kivutio kikubwa kwa wapenzi wa soka na waandishi wa habari waliofika uwanja wa Taifa leo jioni Julai 13, 2017, ambapo timu hiyo ilifanya mazoezi mepesi "nyuma ya pazia" kwani waandishi wa habari an wapiga picha hawakuruhusiwa kuona mazoezi hayo muda wote kwani walipewa dakika 15 tu kupiga picha na kutolewa nje ya uwanja.
Ulinzi uliimarishwa na vyombo vya dola vya kila aina hapa nchini vilionekana vikiwa "bize" kuhakikisha mambo ya kiusalama yanakwenda sawa.
Kwa mujibu wa watayarishaji wa pambano hulo, SportsPesa, pambano litaanza majira ya kioni saa 11 juu ya alama.
Hii ni mara ya kwanza baada ya kupita miongo kadhaa kwa timu ya daraja la kwanza kutoka ligi kuu ya Uingereza kucheza kwenye ardhi ya Tanzania na kubwa zaidi ni kipenzi cha mashabiki wengi wa soka mwanandinga Wayne Rooney ambaye atacheza kwenye ardhi ya "Bongo:.
 Ulinzi uwanja wa Taifa wakati wa mazoezi hayo ya Everton.
 Mashabiki wa Everton na bendera yao
 Mazoezi ya viungo yakiendelea.
 Mashabiki wa Everton wakipiga picha na vijana wa Kimasai waliokuwepo uwanjani kupamba uafrika wetu.Afisa wa SportsPesa, akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment