Monday, 17 July 2017

DSC_0014
Eneo la mto Nyakasangwe lililopo kaika kata ya Bunju linavyoonekana kuharibika vibaya kutokana na uchimbaji wa mchanga , na kupelekea makazi ya wananchi kuwa hatarini.
DSC_0025
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina  akizungumza na vyombo vya habari baada ya kukamilika kwa zoezi la kukagua mto Nyakasangwe, uliopo katika kata ya Bunju ulioharibiwa vibaya na uchimbaji wa mchanga.
DSC_0044
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Mwandishi wa Habari wa kituo cha Radio cha Efm kinachopatikana katika masafa ya 93.7 katika jiji la Dar es Saalam alipokuwa akimuuliza maswali kuhusu uchafuuzi wa mazingira utokanao na uchimbaji wa mchanga katika eneo la Boko.
……………………………………………………………….
NA; EVELYN MKOKOI
NAIBU  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga  Mpina ,amesitisha uchimbaji na uchotaji wa mchanga kiholela katika maeneo yasiyo rasmi.
Pia ametoa siku 30 kwa Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kubaini na kutenga maeneo ya uchimbaji ya mchanga ambayo yapo ndani ya manispaa zao yatakayo ruhusiwa kwa zoezi hilo kisheria.
Akitoa agizo hilo Dar es Salaan leo,wakati wa ziara ya kutembelea Mto Nyakasangwe uliopo maeneo ya Boko Kata ya Bunju alisema kama kuna maeneo ambayo wananchi wanaweza kufika Kwa urahisi, manispaa zinapaswa kuyatembelea maeneo hayo na kuyabaini kama kunauwezekano wakuchimba mchanga.
Alisema ndani ya mwezi mmoja manispaa hizo zinatakiwa  kuandaa utaratibu mfupi wa kutenga maeneo hayo ikiwemo utoaji wa vibali kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Halmashauri pamoja na Nemc.
“Halmashauri zote zilizo na eneo ambalo linaweza kuruhusiwa kuchota mchanga hakikisheni mnatembelea maeneo hayo na kufata taratibu zote za utoaji wa vibali ambapo maeneo mengine yawe ya uchotaji wa mchanga,”alisisitiza Mpina
Alisema watafanya Operasheni ya  usiku na mchana kuhakikisha watu watakaoendelea kuchimba  mchanga na kuchota mchanga sehemu ambazo haziruhusiwi watachukuliwa  hatua ikiwa ni pamoja na kutozwa faini zilizopo kisheria na kufikishwa mahakamani.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunju Bw. Kateni Nassor Msangi alimshukuru Mpina kwa kufanya ziara katika eneo hilo na kuiomba serikali kufanya utaratibu wa kujengea mawe katika kuta za kingo yam to huo ambao umeharibika vibaya, ili kuweza kunusuru mazingira ya mto huo kuharibika pamoja na kunusuru makazi yao.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment