Tuesday, 11 July 2017

 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, akizunhuzma na waandishi wa habari makao makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam leo Julai 11, 2017. Pamoja na mambo mengine, Bw. Kayombo alisema Mamlaka hiyo imekusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 14.4 kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAMLAKA ya Mapato Tanzania, (TRA), imekusanya kiasi cha shilingi Trilioni 14.4 kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi, Bw. Richard Kayombo, amewaambia waandishi wa habari leo Julai 11, 2017.
Bw. Kayombo alisema makusanyo hayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 7.67 ikilinganishwa na makusanyo ya mwaka 2015/2016 ambayo yalikuwa ni kiasi cha shilingi Trilioni 13.3.

Aidha kwa niaba ya Mamlaka, Bw. Kayombo amefurahishwa na muitikio wa wananchi katika kulipa kodi ya majengo na kwa wale wanaoendeleakujitokeza katika ofisi za TRA kote nchini kulipa kodi hiyo ambayo mwisho wa kulipa kodi hiyo kwa mwaka wa fedha unaoishia Julai ni tarehe 15/07/2017.

. “Mwaka wa fedha umeshaanza, wananchi wanaweza kuanza kulipa kodi hiyo sasa, na hii itasaidia kuondoa usumbufu, maana viwango vya kodi ya majengo vinajulikana.” Alisema Bw. Kayombo.
Kuhusu matumizi ya risiti za kielektroniki, Bw. Kayombo ametoa wito kwa wafanyabiashara kote nchini kutoa risiti za EFD pindi wanapouza bidhaa au kutoa huduma na wananchi wote kuhakikisha wanadai risiti za EFD pindi wanaponunu bidhaa au huduma na kwa kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekutwa na kosa la kutokutoa risiti.
“ Hivi sasa kuna zoezi la uhamasishaji na ukaguzi linaloendelea nchi nzima katika sehemu zote za biashara kukagua wafanyabiashara wasiotumia Mashine za Risiti za Kielektroniki za EFDs pamoja na wananchi wote wasiodai risiti baada ya kununua bidhaa au huduma.” Afafanua. Na kuongeza, Napenda kuwakumbusha wananchi wote kuhakiki risiti zao ili kuona usahihi wake ikiwa ni pamoja na tarehe, na mkiasi walicholipa kabla ya kuondoka na risiti hiyo.” Alisisitiza.
 

 Waandishi wa habari wakimsikiliza Bw. Kayombo, (kulia)
 Waandishi wakiwa kazini.
 Bw. Kayombo akiendelea kufafanua masuala mbalimbali yahusuyo kodi.
 Mwandishi wa habari mwandamizi wa Channel 10, Bw. Kibwana Dachi, akirekodi taarifa ya Bw. Kayombo.
 Bw. Dachi, akiuliza swali.
 Afisa Habari Mwandamizi wa TRA, Bi. Rachael Mkundai, (katikati), Afisa Habari, Bi.Mariam Mwayela, (kulia), na Afisa msaidizi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka hiyo, Bw.Chama Siriwa, wakijadiliana jambo.
 Waandishi wa habari, wakiwa makini kazini.Reactions:

0 comments:

Post a Comment