Saturday, 22 July 2017


Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Bw.Sabasaba Moshingi (kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, (ZSSF) Bw.Mwadini Makame, wakitiliana saini mkataba utakaowawezesha wanachama wa ZSSF kupata mikopo kupitia TBP. Halfa ya utilianajisaini mkataba huo imefanyika leo Julai 22, 2017 mjini Unguja.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Bnkiya Posta Tanzania, (TPB), Bw.Sabasaba Moshingi (watatu kushoto), akibadilishana nyaraka za mkataba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, (ZSSF) Bw.Mwadini Makame, (watatu kuli), katika hafla fupi iliyofanyika mjini Unguja leo Julai 22, 2017. Mkataba huo utauwezesha Wanachama wa Mfuko huo kukopa.
Maofisa wa TPB  wakifuatilia mkutano huo wa utilianaji saini ya kutowa mikopo kwa Wanachama wa ZSSF Zanzibar kupitia benki hiyo hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za ZSSF Kilimani Zanzibar.
Maofisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF wakifuatila mkutano huo wa utilianaji wa saini.
Afisa Mawasiliano wa Tpb Bank Chichi Banda akitowa nafasi kwa waandishi wa habari kuuliza maswali wakati wa hafla hiyo.
Bw.Moshingi, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utilianaji  saini kuelezea madhumuri ya hafla hiyo kuwanufaisha Wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar kupata mikopo kupitia Banki yake Tpb Bank. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Mwadini Makame
akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makubaliani ya kupata mikopo kwa Wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, kupitia Banki ya TPB.
Maofisa wa Tpb Bank wakifuatilia hafla hiyo ya utilianaji wa saini na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF. 
Mwandishi wa habari akiulisa swali wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini baina ya ZSSF na TPB, kutowa mikopo kwa Wanachama wa ZSSF kupata Elimu ya Juu na Mkopo wa kuazia maisha
Mwandishi wa habari akiuliza swali wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mikopo wa TPB. Bw.
 Henry Bwogi, (kushoto), akifafanua na kujibu maswali yalioulizwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya utilianaji wa saini baina ya pande hizo mbili. 
Afisa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Bi Raya Hamad Khamis akitowa shukrani kwa washiriki wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini uliofanyika katika Ofisi za Jengo la ZSSF Kilimani Zanzibar. 
Viongozi wa Tpb Bank na ZSSF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa hafla hiyo. 
Bw.Moshingi, (kushoto), akiwa na Maofisa wa ZSSF wakibalishana mawazo baada ya kumaliza hafla ya utilianaji wa saini na ZSSF, katikati Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ZSSF Ndg.Mwadini na Afisa wa ZSSF Miradi Ndg. Muumin.
Bw. Moshingi akifurahia jambo na maafisa wa ZSSF baada yahafla hiyo. (NA Othman Mapara.Blogspot.com
Zanzinews.com).
Reactions:

0 comments:

Post a Comment