Sunday, 16 July 2017
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi Wateja wake Mikoa ya
Dodoma, Singida, Manyara, shinyanga, Tabora, Mwanza, Musoma na baadhi ya maeneo ya Arusha kwa katizo la umeme lililotokea majira ya saa 7:34 Mchana, leo Jumapili Julai 16, 2017
Sababu ni kutokea kwa hitilafu katika mfumo wa Kilovolti 220 kituo cha kupooza na kusambaza umeme Dodoma.
Mafundi walifanya jitihada za kurudisha umeme katika hali ya kawaida, na hivi sasa Mikoa yote inapata umeme
Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo:
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu Julai 16, 2017
Reactions:

0 comments:

Post a Comment