Sunday, 2 July 2017

 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MENEJA uhusiano wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, (NIDA), Bi. Rose Mdami, amewaondoa hofu wananchi kuwa vitambulisho vya taifa ni halali kutumika kwenye taasisi za (Benki) na kwingineko (benki). kwani tayari NIDA imekwishatoa muongozo wa kimfumo kwenye mabenki hayo. "Tumeshaweka mfumo maalum kwenye mabenki ambayo yalikuwa yanasita kuvitambua vitambulisho vya taifa kwa madai ya kutokuwepo kwa saini na alama nyingine, lakini mfumo tuliowapatia wanaweza ku-access taarifa zaidi za muhusika au mmiliki wa kitambulisho ikiwa ni pamoja na wapi alikozaliwa, anakoishi na kazi anayofanya lakini zaidi ya hayo hata saini ya mwenye kitambulisho wanaweza kuiona." Alisema Bi Mdami. kwenye mahojiano maalum na K-VIS BLOG kwenye banda la NIDA lililoko kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Julai 1, 2017. Wakati akizungumza hayo ni dhahiri ukifika kwenye banda la Mamlaka hiyo utaelewa kuwa uhitaji wa vitambulisho vya taifa miongoni mwa wananchi ni mkubwa mno. Mamia ya wananchi wamekuwa wakifurika kwenye banda hilo ili kupata huduma ya vitambulisho vya taifa ambapo licha ya NIDA kutenga maeneo mawili kwa ajili ya wananchi kupatiwa huduma hiyo bado imeonekana kuwa hapatoshi na sasa wananchi wamejazana kwenye korido za banda hilo na hata wakati mwingine askari wanalazimika kusimamia utaratibu.
Tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameyafungua rasmi maonesho hayo na wananchi wanazo takriban siku sita kujipatia huduma hiyo muhimu. Pichani wananchi wakiwa wamejazana kwenye banda la NIDA Julai 2, 2017.
 Afisa wa NIDA, (kulia), akimsikilzia mwananchi huyu aliyefika kujipatia huduma ya kitambulisho cha taifa. K-VIS Blog ilifanikiwa kumsikiliza akijitambulisha kuwa anatoka Zanzibar.
 Afisa wa NIDA, akitoa maelekezo kwa wananchi hawa waliofika kupatiwa vitambulisho vya taifa
 Mwananchi (kulia), akimsikilzia afisa huyu wa NIDA, wakati alipofika kupatiwa huduma ya kitambulisho cha taifa
Afisa wa NIDA, akisoma fomu ya maombi ya kitambulisho cha taifa iliyojazwa na mmoja wa wananchi hawa waliofika kupatiwa huduma ya kitambulisho cha taifa.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment