Thursday, 27 July 2017

Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini,Joseph Msukuma akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Ihanamilo Kata ya Nkome wakati za zoezi la kuondoa Vigingi ambavyo viliwekwa kwenye eneo ambalo limetengwa kwaajili ya ujenzi wa Stendi ya mabasi kijijini Hapo.
Wananchi wakishiriki zoezi la kuondoa vigingi ambavyo vilikuwa vimewekwa na mnunuaji wa eneo hilo kwaajili ya matumizi ya kituo cha mafuta.
Mbunge wa Jimbo hilo,Joseph Kasheku Msukuma akiondoa kigingi ambacho kilikuwa kwenye eneo hilo akishirikiana na wanakijiji wa kijiji cha ihanamilo.
Kahimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita akielezea juu ya utatuzi wa tatizo ambalo limeonekana kwenye kijiji hicho juu ya kuuzwa kwa eneo ambalo lilikuwa limetengwa kwaajili ya matumizi ya stendi.

Mbunge Joseph Msukuma akiwa na mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw Thomas Alila wakati alipokuwa akimuuliza juu ya kwanini wameamua kuuza eneo ambalo lilitengwa kwa matumizi ya stendi.

Moja kati ya wananchi wa kijiji hicho,Bw Revocatus Faustine akimueleza mbunge kutokuwepo kwa makubaliano ya kuuzwa kwa eneo la stendi kwaajili ya ujenzi wa madarasa
Wananchi wakifuatilia mkutano.
Diwani wa Kata ya Nkome Masumbuko Sembe akiulizwa juu ya kushiriki kwenye uhuzwaji wa eneo hilo.
Mbunge Msukuma akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho. (PICHA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLIE)
Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Mh,Joseph Kasheku Msukuma  ambaye pia ni mwenyekiti wa  chama cha mapinduzi CCM Mkoani Geita
ameongoza mamia ya wananchi wa kijiji cha Hiyanamilo Kata ya Nkome Wilayani
Geita kutoa visiki ambavyo viliwekwa na mtu ambaye inasadikika amenunua eneo la
kijiji   linalokadiliwa kuwa ni hekari
moja na nusu  ambalo lilitengwa kwa
matumizi ya stendi kutoka kwa serikali ya kijiji.
 
Hatua hiyo
imekuja  baada ya Serikali ya Kijiji
ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho ,Bw Thomas Alila na mtendaji wa kijiji
Charles Mbilingi kuuza eneo kwa kiasi cha sh ,Milioni sita (6).
 
Kwa maelezo
ya afisa mtendaji wa Kijiji Charles Mbilingi amesema kuwa tarehe 15 mwezi huu
walikaa kwenye kikao na wanakijiji na kuamua kwamba wauze eneo hilo  ili liweze kusaidia ujenzi wa shule.
 
“Tulikaa
kama halmashauri ya Kijiji tukajadili namna ya kutatua changamoto ya kukosekana
kwa shule kwenye kijiji chetu tulipojadili tukaonelea kwa sababu tuna eneo ni
bora tuliuze ili tuweze kupata pesa ambazo zitasaidia ujenzi wa madarasa na
hatukufanya peke yetu 
tuliwashirikisha wananchi wa kjiji wakawa
wamekubali”Alisema Mtendaji.
 
Hata Hivyo
kutokana na maelezo hayo ya mtendaji wa Kijiji Mbunge  Msukuma amewaeleza wananchi ambao walikuwa
kwenye Mkutano wa hadhara kuwa eneo hilo liliuzwa tarehe tano mwezi huu jambo
ambalo yeye alilikataa kutokana na faida ambazo zinaweza kupatikana kutokana na
uwepo wa eneo hilo.
 
“Nimesikitishwa
sana na kitendo ambacho kimefanyika cha kuuzwa eneo hilo kiasi cha Shilingi
milioni sita (6) na mimi nilimpigia simu mtendaji nikamwambia  azirudishe pesa aende halmashauri kuna
maelekezo kwa mkurugenzi na tutambue kuna maeneo muhimu lazima yawepo
leo(jana)ninakwenda kung’oa visiki vyote”Alisema Msukuma
Katika hali
isiyo ya kawaida  Diwani wa Kata ya Nkome
Masumbuko Nsembe amejikuta jina lake likiwa limeandikwa kuwa ni miongoni kati
ya viongozi ambao walilidhia  kuuzwa kwa
eneo  la kijiji.
 
“Mheshimiwa
Mbunge mimi sikuuza nilifika saa kumi na moja nilikuta wakisoma hiyo taarifa ya
kuuza lakini mimi niliwaambia kuwa wasiuze eneo hilo kwa hicho kiasi.”Alisema
Diwani
 
Katika hali isiyo
ya kawaida wananchi ambao walihudhuria  kikao
hicho cha kukubaliana kuuzwa kwa eneo hilo  walipotajwa majina yao walijikuta wakidai
kushindwa kujua hali hiyo imetokana na nini na kama waliingizwa mkenge kwenye
mauziano hayo.
Kutokana na
hatua ambayo mbunge ameifanya ya kuongeza wananchi kutoa visiki wananchi
wameshukuru na kusema kuwa walikuwa hawajui
kama eneo lao limeuzwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment