Wednesday, 12 July 2017


Mkuu wa Kivuko cha Magogoni/Kigamboni Mhandisi Lukombe King’ombe akizungumza na waandishi wa Habari wa TBC1 waliotembelea kivuko hicho leo asubuhi na kufanya nae mahojiano ya moja kwa moja kupitia kipindi cha Jambo Tanzania.Abiria wakiwa wamevalia maboya maalumu ya kujiokolea ndani ya Boti ya MV. Mkongo inayosimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA). Boti hiyo inatoa huduma za usafiri katika mto Rufiji kati ya Utete na Mkongo wilayani Rufiji Mkoani Pwani.Muonekano wa Boti ya MV. Mkongo ikiwa imepaki kusubiria abiria katika eneo la Mkongo. Boti hiyo inayosimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) inatoa huduma zake katika mto Rufiji kati ya Utete na Mkongo wilayani Rufiji mkoani Pwani.Boti za raia zilizokua zikitumika kuvusha abiria katika Mto Rufiji kati ya Utete na Mkongo kabla ya ujio wa Boti ya MV. Mkongo kuletwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) zikiwa zimepakia abiria tayari kwa kuanza kuwavusha.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment