Wednesday, 5 July 2017

 Meneja Mikopo wa Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Bi.Joanitha Deogratius (kulia), akimuhudumia askari polisi, Felista Elais, aliyefika kufungua akaunti kwenye banda la Benki hiyo, jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Julai 5, 2017 ambako maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanaendelea. Mamia ya wananchi wamejitokeza kufungua akaunti TPB ambapo kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mikopo wa benki hiyo, alisema wananchi wanakaribishwa kukopa kwenye benki hiyo ilimradi wakiwa wamejiunga kwenye vikundi, lakini pia kwa wale wanaotarajia kustaafu,  wanaalikwa kuomba mikopo  TPB, ambapo Mkurugenzi wa Mikopo, benki hiyo, Bw. Henry Bwogi alisema, benki imeanzisha mikopo maalum kwa wataafu. "TPB kwa kushirikiana na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ya PSPF, PPF, NSSF, ZSSF, LAPF na HAZINA inatoa mikopo maalum ili kuwawezesha wastaafu waweze kukidhi mahitaji yao kwa wakati wanaohitaji." Alisema. Bw. Bwogi. Alisema wenye sifa za kupata mikopo hii ni pamoja na wastaafu wanaopitishia pensheni zao kutoka kwenye taasisi za Mifuko ya Pensehni, ambapo utaratibu wa makato ya marejesho utakuwa umewekwa baina ya Benki ya Posta na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Wastaafu wa wizara ya Fedha. (NA K-VIS BLOG/Khalfan Said)
 Mkurugenzi wa Mikopo wa TPB, Bw. Henry Bwogi, (kulia), akizunuzma na Waandishi wa habari kwenye banda la benki hiyo leo Julai 5, 2017
 Afisa wa polisi akimsikilzia kwa makini meneja mikopo wa TPB, Bi.Joanitha Deogratius kuhusu utaratibu wa kufungua akaunti na kupata mkopo
 Baada ya kuelewa utaratibu wa kufungua akaunti na upatikanaji wa mikopo, sasa ni nyuso za tabasamu na furaha kati ya Bi. Joanitha(kulia) na Afisa wa polisi Felista.
 Afisa w aTPB, Bw.Godbright Mlay, akiwa kazini kwenye banda la TPB.
 Mteja wa TPB, akipatiwa huduma za kibenki kwenye banda la TPB Leo Julai 5, 2017. Kulia ni Mtoa huduma (Teller), Bi, Shufaa Mohammed.
 Meneja mikopo wa TPB, Bi. Joatha Deogratius (kushoto) na Afisa Mauzo wa benki hiyo, Bi.Heavelight Uisso, (wapili kushoto), wakiwahudumia wateja hawa waliofika wkenye banda la TPB leo Julai 5, 2017.
Kikosi kazi cha TPB kikiongozwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa benki hiyo, Bi. Chichi Banda, (wapili kulia), kilichoko kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment