Sunday, 9 July 2017

Afisa wa Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi Hifadhi ya Jamii,(SSRA), Bi. Imani Masebu, (katikati), akizunguzma na Meneja Matekelezo wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena, (katikati), na Afisa Uhusiano Mwandamizi, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati wa maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, leo Julai 9, 2017. SSRA imesogeza huduma kwa wadau wa Mfuko huo ambapo maafisa wake wamewekwa kila banda mshirika wa Mamlaka hiyo ikiwemo WCF na PSPF ili kujua kero za wananchama.
Afisa wa SSRA Bw. Mashala Bukalasa,(kulia), akimuhudumia mwananchi aliyetembelea banda la LAPF kwenye maonesho ya 41 ya biashaya ya kimataifa ya Dar es Salaam.


 Afisa Mwandamizi wa Huduma za Sheria kutoka SSRA, Bw. Omary Halfan akisikiliza kwa makini hoja za mmoja wa wadau wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii alietembelea Banda la NSSF kwenye Maonesho ya Sabasaba
 Maafisa wa SSRA Bw. David Lyanga na Imani Masebu wakijibu hoja mbalimbali za wadau waliotembelea banda la PSPF wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam

kurugenzi wa Fedha, Mipango na Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka SSRA Bw. Mohamed Nyasama akibadilishana mawazo ya maafisa kutoka na SSRA na GEPF alipotembelea banda la GEPF kwenye Maonesho ya Sabasaba
Reactions:

0 comments:

Post a Comment