Sunday, 2 July 2017

 Afisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, (NIDA), kulia, akitoa matangazo kwa wananchi waliofurika nje ya hema la Jakaya Kikwete, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, ambako kunafanyika maonesho ya 41 ya biashara yab Kimataifa ya Dar es Salaam.
Meenja Uhusiano wa NIDA, Bi. Rose Mdami, (kulia), akitazama nyaraka za wananchi hawa ambao walifika kuomba watengenezewe vitambulisho vya taifa.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WANANCHI wamezidi kumiminika kwenye banda la Mamlaka ya vitambulisho vya taifa, (NIDA), lililoko kwenye hema la Jakaya Kikwete, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, ambako kunafanyika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa, maarufu “Sabasaba”.
Banda la NIDA, limekuwa ni moja ya mabanda yanayojaa watu muda wote hali inayowafanya wananchi “kudamkia” (kufika asubuhi na mapema punde tu milango ya viwanja hivyo inapofunguliwa.
Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa NIDA, Bi.Rose Mdami, wananchi wanatakiwa kuja na nyaraka muhimu ili kujipatia vitambulisho kwa haraka. “Naomba mnisikilize, kila mtu aliyefika hapa kwa hitajio la kutengenezewa kitambyulisho cha taifa, yampasa kuja na vielelezo muhimu na kama unavyo vya ziada itakuwa rahisi kuhudumiwa muhimu zaidi uwe na cheti cha kuzaliwa, na utakapofika hapa unapaswa kukionyesha cheti hicho kwa afisa wa uhamiaji ambaye atakithibitisha kabla ya kujaza fomu na hatua kwa hatua inayofuata.” Alsiema Bi. Mdami.
Maonesho hayo ambayo yalianza Juni 28, yalipangwa kufikia kilele Julai 8, lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, aliongeza siku tano zaidi za maonesho hayo kuendelea na hivyo yatafikia kilele Julai 13, 2017. Tayari Mamlaka ya Ukuzaji Biashara (Tan Trade) ambao ndio wenye dhamana ya kuandaa maonesho hayo imeanza kutoa matangazo kwa wananchi kuhusu agizo hilo la Rais.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment