Thursday, 8 June 2017Mhe.Mpango
Waziri wa Fedha na Mpango Mhe.Dr.Philip Mpango akiwaonyesha waandishi wa Habari mkoba wenye hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th June 2018.
Dk Mpango
Waziri wa Fedha na Mpango Mhe.Dr.Philip Mpango akiwasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18.
IMG_7397
Wabunge wakiingiaUkumbiwa Bunge kusikilizahotubayabajetiyaSerikalikwamwaka 2017/2018 leoBungeniMjini Dodoma tarehe 8th June 2018.
IMG_0651
Wabunge wakisikilizahotubayaBajetiyayaBajetiyaSerikalikwamwaka 2017/2018 leoBungeniMjini Dodoma tarehe 8thJuni 2018
*YALIYOJIRI KATIKA HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO,MHE. DKT. PHILIP I. MPANGO (MB),AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2017/18*

#Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi tano za Afrika zilizoongoza kwa kuwa na kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi-Mhe. Dkt.Philip Mpango

#Kwa mujibu wa jarida la Benki ya Dunuia uchumi wa Taifa ni imara-Mhe. Dkt.Philip Mpango

#Serikali imepunguza riba ambazo benki za biashara hukopa kutoka Benki Kuu kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 12.0-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali imezifungia Benki tatu za biashara za Twiga,FBME Bank Ltd na Mbinga Community Bank-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Kuanzia Julai 2016 hadi Machi,2017 jumla ya biashara 7,277 zilifungwa katika mikoa mbalimbali nchini-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Katika kipindi cha Julai 2016 mpaka Machi 2017,biashara mpya zipatazo  224,738 zilisajiliwa-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Tanzania ni nchi ya 132 Duniani  kwa urahisi wakufanya biashara ikiwa imepanda kwa nafasi 12 kutoka nafasi ya 144 mwaka 2016-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Tanzania imekuwa nchi ya kwanza miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki kwa kuvutia uwekezaji na ya nane kwa Afrika-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Nikinyume na sheria na utaratibu kwa watumishi wa TRA kutumia vitisho na unyanyasaji kwa walipa kodi,kuwadai rushwa au kuwazidishia makadirio ya kodi-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Tunawaomba wananchi kutupatia taarifa kuhusu wafanyabiashara wanaokwepa kodi-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Katika kipindi cha Julai 2016 hadi Aprili 2017 mapato kutoka vyanzo vyote yalifikia Shilingi bilioni 20,710.5-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali imeendelea kuboresha mifumo ya  kielektroniki katika ukusanyaji mapato ili kudhibiti upotevu wa mapato-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#TRA imekusanya Shilingi bilioni 15,134.2 kama kodi ya majengo kwa kipindi cha Octoba 2016 hadi Mei,2017-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Katika kipindi cha Julai,2016 hadi Aprili,2017 jumla ya Shilingi bilioni 203.0 zimetolewa kugharamia elimu bila malipo-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Hadi Machi 2017,deni la Taifa lilifikia Shilingi bilioni 50,806.5-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Deni la Serikali limeongezeka kwa asilimia 9.2 kutoka Shilingi bilioni 39,274.6 Machi 2016 hadi shilingi bilioni 42,883.6 Machi,2017-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Tanzania bado ina uwezo wa kuendelea kukopa kutoka ndani na nje ya nchi na pia ina uwezo wa kulipa mikopo inayoiva kwa kutumia mapato yake ya ndani na nje-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali itarasimisha sekta isiyo rasmi ili iweze kuingia katika mfumo wa kodi-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali itarasimisha miliki za ardhi kwa lengo la kuongeza mapato-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali itaendelea kudhibiti na kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serili imezindua mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki ambao utadhibiti udanganyifu-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali kuwapatia vitambulisho wafanyabiashara wadogowadogo wasio rasmi-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali kutoruhusu usafirishaji wa madini kutoka migodini na kupeleka moja kwa moja nje ya nchi-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa za mtaji-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha asilimia sifuri katika huduma zinazotolewa kwenye usafirishaji wa mizigo nje ya nchi-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Mabadiliko ya ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji baridi kutoka shilingi 58 kwa Lita hadi shilingi 61-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Mabadiliko ya ushuru wa bidhaa kwenye bia nyingine zote kutoka shilingi 729 kwa Lita hadi shilingi 765 kwa lita-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali kufuta Ada ya Mwaka ya Leseni ya Magari iliyokuwa inalipwa kwa magari yasiyotumika-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Ada ya Leseni ya Magari italipwa Mara moja tu gari linaposajiliwa-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali imeshusha ushuru wa mazao kutoka asilimia 5 hadi asilimia 3-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Mtu anayesafirisha mazao kutoka halmashauri moja kwenda nyingine yasiyozidi tani moja asitozwe kodi-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye viunganishi vya pikipiki-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali kufuta ada ya ukaguzi wa viwango kwa mazao ya biashara kama pamba,kahawa,chai,korosho inayotozwa na Shirika la Viwango Tanzania-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali kufuta Ushuru wa Huduma kwenye nyumba za kulala wageni-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali kufuta ushuru wa Mabango kwa mabango yanayoelekeza mahali huduma za jamii zinapopatikana-Mhe. Dkt.Philip Mpango

#Serikali kufuta ada ya makanyagio minadani-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Sura ya Bajeti inaonesha kuwa jumla ya shilingi bilioni 31,712.0 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika kipindi cha mwaka 2017/18-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia shilingi bilioni 3,971.1 ambayo ni asilimia 12.5 ya bajeti yote-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Serikali inatarajia kukopa shilingi bilioni 7,763.9 kutoka soka la ndani na nje kwa masharti ya kibiashira-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Shilingi bilioni 19,712.4 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida-Mhe.Dkt. Philip Mpango

#Shilingi bilioni 7,205.8 kwa ajili ya mishahara-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Shilingi bilioni 9,461.4 kwa ajili ya kulipia deni la umma na huduma nyinginezo-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Shilingi bilioni 11,999.6 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo sawa na asilimia 38 ya bajeti yote-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Bajeti hii inalenga kujenga msingi madhubuti wa uchumi wa viwanda na kupanua fursa za ajira na biashara-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Dhamira yetu sote ni kufikia kiwango cha uchumi wa kipato cha kati ifikapo 2025-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Kufanikiwa kwa bajeti hii kunahitaji nidhamu ya hali ya juu katika usimamizi wa mapato na matumizi-Mhe. Dkt. Philip Mpango

#Natoa rai kwa kila Mtanzania kutimiza wajibu wake ili Bajeti hii iweze kutekelezwa kama ilivyopangwa-Mhe. Dkt. Philip Mpango*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO*


Reactions:

0 comments:

Post a Comment