Sunday, 4 June 2017

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe kushoto akimkabidhi Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale tuzo ya mshindi wa banda bora la sekta ya nishati na mazingira katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara wakati jijini Tanga. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella.
 Waziri wa Malisili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto)
akifurahia jambo na
 
Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale mara baada ya kumkabidhi tuzo ya mshindi wa banda bora la sekta
ya nishati na mazingira katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara wakati alipokwenda kuyafunga jijini Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella.
 Watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakionyesha tuzo ambazo Sirika hilo lilitunukiwa kwenye maonesho hayo
 Watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (TPDC) wakiongozwa na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Augustino Kasale kulia na katikati ni Mwanasheria wa TPDC, Kelvin Gadi wakiwa na tuzo yao waliyoipata
 Mkuu wa wilaya ya Tanga, Mhe.Thobias Mwilapwa, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kulia ni Mwanasheria wa
Shirika hilo, Kelvin Gadi
 Mwanasheria wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kelvin Gadi (kulia), akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martine Shigella (ushoto)
 Mkuu wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Mhe.Godwin Gondwe (wa pili kulia)  akizungumza jambo na watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) mara baada ya kulitembelea banda la Shirika hilo.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Mhe.Godwin Gondwe (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja  na watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). (Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha).
Reactions:

0 comments:

Post a Comment