Thursday, 15 June 2017

TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Yanga inapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa zisizo rasmi zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari juu ya mchezaji wetu Simon Msuva.
Taarifa hizo za upotoshaji zinadai mchezaji husika amevunja mkataba wake na Yanga kitu ambacho si kweli.
Kama klabu tunapenda kuwataarifu kwamba, klabu bado ina mkataba mrefu na Simon Msuva. Tunafahamu kuna vilabu vingi vinamtaka mchezaji wetu kutokana na ubora wake na sisi kama klabu hatuna pingamizi.
klabu yoyote ndani ya nchi na nje ya nchi inayomtaka Simon Msuva inakaribishwa klabuni na kufuata taratibu zote sahihi za kumnunua mchezaji. Bado Msuva ni muhimu katika klabu yetu na sisi tunapenda sana kuendelea nae lakini hatuwezi kumzuia kutafuta riziki sehemu bora zaidi kuliko kwetu.
Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano Yong africans sports club. 15-06-2017.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment