Monday, 5 June 2017
Mshambuliaji wa Singida Utd, Nhivi Simbarashe (wa pili kulia) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa AFC Leopards, Joshua Mawira, (kulia) wakati wa mchezo wa fungua dimba mashindano ya SportPesa Super Cup, yaliyoanza leo kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Wa pili (kushoto) ni  Marcus Abwao.  Katika mchezo huo uliomalizika hivi punde AFC Leopard wameibuka kidedea kwa ushindi wa penati 5-4 baada ya kumalizika dakika 90 zikiwa sare ya 1-1. Mchezo unaofuata hivi punde ni Yanga vs Tusker


Mshambuliaji wa Singida Utd, Nhivi Simbarashe (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa AFC Leopard ya Kenya, Joshua Mawira, wakati wa mchezo wa fungua dimba mashindano ya SportPesa Super Cup, yaliyoanza leo Juni 5, 2017 kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. (PICHA NA MUHIDIN SUFIANI)Wachezaji wa AFC Leopards, wapigwa na butwaa baada ya kufungwa bao katika dakika ya 10 kipindi cha kwanza.


Mchezaji wa Singida United, Mtasa Wisdom, akiruka kuokoa katikati ya wachezaji wa AFC Leopards.


Hatari langoni mwa AFC Leopard


Reactions:

0 comments:

Post a Comment