Friday, 9 June 2017

http://www.tamisemi.go.tz/noticeboard/tangazo-1068-20170609-Uchaguzi-kujiunga-kidato-cha-5-vyuo-vya-ufundi-2017/

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene, amesema jumla ya wanafunzi 93,019 waliohitimu kidato cha nne mwaka 2016, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ufundi kwa mwaka wa masomo wa 2017.
Mhe. Simbachawene ametoa taarifa hiyo leo Juni 9, 2017 mbele ya waandishi wa habari mjini Dodoma.
Alisema kuwa kati ya wanafunzi 96,018 ni wanafunzi 93,019 ndiyo wenye sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ufundi kwakuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi.
“Kati ya wanafunzi hao 92,998 ni wa shule (School Candidates) na wanafunzi 21 walisoma chini ya taasisi ya elimu ya watu wazima”alisema Simbachawene.
Aliongeza kuwa jumla ya watahiniwa wa shule 349,524 wakiwemo wasichana 178,775 sawa na asilimia 51.1 na wavulana 170,749 sawa na asilimia 48.9 walifanya mtihani huo mwaka 2016.
Aidha Mhe. Waziri amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati, endapo watachelewa kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya kufungua shule nafasi zao itachukuliwa na mwingine.
“Tarehe ya kuripoti katika muhula wa kwanza kwa kidato cha tano kwa mwaka 2017 utaanza Julai 17, 2017 lakini kwa wanafunzi wanaoingia kidato cha sita watafungua tJulai 3, 2017 kama ilivyokuwa imepangwa”alisema.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment