Monday, 5 June 2017NA K-VS BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI
JUMUIYA ya nchi za Kiarabu, zikiongozwa na Saudi Arabia, U.A.E, Misri, Bahrain, Yemen na Maldives wamevunja uhusiano na Qatar kwa kile kilichoelezwa kuwa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa gesi linafadhili vitendo vya kigaidi hususan kundi la IS.
Qatar imekanusha vikali tuhuma hizo na kusema uamuzi wa mataifa hayo hauna uhalali wowote wa kisheria.
Taarifa ya shirika la habari la Saudi, iliyotolewa leo Jumatatu Juni 5, 2017 imesema imechukua uamuzi huo kwa kulinda usalama wa taifa lake.
Taarifa ya serikali ya Kifalme ya Saudi Arabia, imesema kuwa Qatar inatoa hifadhi kwa idadi kubwa ya magaidi na vikundi vyenye msimamo mkali vinavyokusudia kuondoa utengamano wa kiusalama kwenye eneo lote la Jumuiya ya mataifa ya Kiarabu.
Ikijibu uamuzi huo, Qatar imesema “hakuna uhalali wa kisheria” kwa nchi kadhaa kuondoa uhusiano wa kidiplomasia  na nchi hiyo ya ghuba. Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump aliyoifanya nchini Saudi Arabia.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment