Sunday, 11 June 2017NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
SAIF al-Islam, mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, marehemu Muamar Gaddafi ameachiwa kutoka gerezani chini ya sheria mpya ya msamaha.
Kuachiwa kwake kumethibitishwa na moja ya utawala wa Libya wenye makazi yake kwenye mji wa Mashariki wa Tobruk.
Mahakama ya Tripoli ilimuhukumu al-Islam adhabu ya kifo mnamo mwaka 2015 kutokana na makosa ya jinai vitani (war crimes) na kukandamiza wandamanaji wakati wa uasi wa mwaka 2011 dhidi ya utawala wa baba yake.
Kwa mujibu wa taarifa ya wapiganaji waliokuwa wanadhibiti gereza alilokuwa akishikiliwa al-Islam kwenye kwenye mtandao wa Facebook, na kiongozi wa wapiganaji hao, Abu Bakar al-Saddiq, al-Islam aliachiwa tangu Jumamosi.
Taarifa hiyo ilisema, wameamua kumuachia al-Islam baada ya maombi ya Baraza la Wawakilishi (HoR), bunge lenye makazi yake kwenye mji wa Tobruk.
Mtoto huyo wa Gaddafi, pia anatakwia na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, (ICC).Reactions:

0 comments:

Post a Comment